Translate

Thursday, April 30, 2015

Rais KIKWETE afanya mazungumzo na BILL CLINTON


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kisha kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam
Rais JAKAYA KIKWETE amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa 42 wa MAREKANI - BILL CLINTON ambaye anaendelea na ziara yake nchini. 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU Jijini DSM imesema kuwa wakati wa mazungumzo yao viongozi hao wamezungumzia baadhi ya miradi inayodhaminiwa na kugharimiwa na Taasisi ya CLINTON. 

Miradi hiyo ni ile iliyopo katika sekta ya afya na hasa katika utoaji wa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vinavyosababisha ukimwi, afya za akina mama na jinsi ya kupunguza vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

No comments: