Translate

Friday, July 10, 2015

Nani msafi wa rushwa ndani ya ccm?


pic+vichwa

Vikao vya maamuzi ya CCM vimeanza Dodoma. Huku wanachama na wapenzi wa CCM Macho na masikio yao yakiwa yametegeshwa dodoma kusubiri ni nani atakayeteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa miaka yote ambayo CCM imeshirki chaguzi kama hizi huko nyuma, Ni mwaka huu pekee ambapo CCM imekuwa katika wakati mgumu.

Ugumu huu unatokana na mambo mrngi, Lakini jambo kubwa ni MAKUNDI ya wagombe wa nafasi ya urais, ambayo kwa kiwango kikubwa kinaitishia uhai wa CCM kama vikao hivi havitatumia busara katika hitimisho ya mchato huu.
Siyo mara ya kwanza CCM kuwa na makundi wakati kama huu wa uchaguzi, Bali makundi haya yalikuwepo lakini walikuwa wakifanya kampeni zao kwa kufuata kanuni na taratibu za chama bila ya vitisho au kuchafuana.
Lakini taratibu makundi haya yalianza kushinikiza vikao vya maamuzi kuteuwa wagombea wanaowataka na hata wakati mwingine kutoa vitisho kwa viongozi na wajumbe wa vikao hivi ili mgombea wao ateuliwe.
Kwa mfano kundi la WANAMTANDAO: Kundi hili lilianzishwa na mwaka 1995 likiwa na wagombea EDWARD LOWASA na JAKAYA MRISHO KIKWETE. Baada ya lowasa kuenguliwa katika hatua za awali, kundi hili lilihamishia nguvu zake kwa kikwete,ambapo katika hatua za mwisho, Mkapa aliibuka mshindi na hivyo, akateuliwa kupeperusha bandera ya CCM.
Kwa kumbukumbu zaidi, Mkapa baada ya kuteuliwa na CCM, Aliwaomba wanaCCM wenzake wavunje makundi ili waingie katika kampeni wakiwa wamoja, Na kuonya kwamba kundi hili la wanamtandao ni hatari kwa uhai wa chama.
WANAMTANDAO WALIKUBALI MDOMONI LAKINI MOYONI HAWAKUVUNJA KUNDI LAO.
Taratibu,kundi la wanamtandao likaanza kujiimarisha kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 kwa kuongeza watu katika kundi hili pamoja na kuandaa mpango mkakati utakaowawezesha kushinda uchaguzi wa mwaka huo.
Kwa upande wa mikakati, WANAMTANDAO walianza kuwaweka watu wao katika chaguzi za chama ili wapate idadi itakayowezesha mgombea wao kuteuliwa, KIKWETE.
Kwa kuanzia,wanamtando waliwaweka watu wao katika uchaguzi wa ndani ya chama wa mwaka 1997 na uchaguzi wa mwaka 2002.
Kwa kumbukumbu zaidi, uchaguzi wa nadani ya chama ya mwaka 2002, Kikwete alilalamikia kura za itifaki zilizopigwa katika uchaguzi huo.
Katika kuhakikisha kuwa idadi ya wanamtandao unaongezwa,kundi hili liliwaingiza kundini, wafanyabiasha ,wanachama na viongozi wa CCM ,watumishi wa umma pamoja na watendaji katika vyombo vya dola.
Baadhi ya wanamtandao waliokuwa wanakundi ni: Kikwete, Lowassa, Rostam, Membe, Sitta, Apson Nwang’onda, Kingunge, Sofia Simba, Makala, Karamagi, Chenge, Noni, Diallo, Meghji nk.
Kwa wale wenye kumbukumbu watakubaliana na mimi kuwa, Uchaguzi wa mwaka 2005, Ulitawaliwa na rushwa,kuchafuana miongoni mwa wagombea pamoja na uzushi, vitisho, shinikizo za kila aina,maada mgombea wao ateuliwe.
Ni uchaguzi huu ambapo watanzania tulishuhudia Dr Salim akizushiwa kuwa alimuua Karume,mara Hizbul mara mwarabu.
Sumaye alizushiwa kuwa ameficha fedha nyingi nje ya nchi, Mwandosya akizushiwa kuwa aliiuza TTCL na mtoto wake anasomeshwa na wanunuzi wa TTCL afrika kusini.
Haya yote yalifanyika kwa lengo moja tu!: KIKWETE aingie madarakani kwa namna yoyote ile, iwe kwa uzushi, kwa shinikizo,kwa vitisho au kwa fedha haramu za EPA nk na walifanikiwa, Huku wakiacha maumivu makali kwa washindani wao.
Ni hapo ambapo kundi hili la wanamtandao walijiaminisha kuwa Kile watakacho amua kikitenda kitafanyika kwa matakwa yao.
Ndiyo maana Lowassa alipoongea na wanahabari siku chache kabla ya kutangaza nia, alisema kuwa walikubaliana na Kikwete kuwa kipindi hiki ni kipindi cha Lowassa kuwa rais wa awamu ya tano.
Vivile Mzee Kingunge wakati Lowassa anatangaza nia Arusha alisea”Ni vyema Lowassa wakakaa na Kikwete ili wamalize tofauti zao.
Kwa kuwa kundi hili lilijiapisha kufanya wanayoyataka iwe kwa uhalali au haramu na kujiona kuwa ni wamoja, Walisahau jambo moja muhimu sana, DHAMBI YA UBAGUZI.
Madhara yatokanayo na dhambi hii imefafanuliwa vizuri katika hotuba ya baba wa taifa mwalimu nyere ya mwaka 1995 kilimanjaro hotel,ambpo mwalimu alisema”Dhambi ya ubaguzi ni dhambi mbaya sana, Na ukishaitenda huwezi kuiacha na ni sawa na kula nyama ya mtu”….”Huwezi kutenda dhambi hii halafu ukabaki hivihivi salama”.
Watu wa nchi ile ile mnapoamua kubaguana ukisema sisi ni na wao ni…Na kwamba mkawaacha wenzeni wa wamebung’aa,wao watabaki salama lakini ninyi ….hamtabaki salama”.DHAMBI HII NDIYO INAWATAFUNA WANAMTANDAO MPAKA LEO.
Kwa nini nasema hivyo?.Unapokuwa ukiwachambua watia nia wa CCM,Utagundua kwamba,Ni wanamtandao walewale ambao sasa wamemeguka na kuwa vimtandao, Na kwamba,Ndio wanaokashifiana ,kuzushiana na kuchafuana maadam mtu wao ateuliwe na CCM.
Hii inaonyesha kuwa wanamtandao waliomzushia na kumchafua salim hawapo pamoja kama walivyokuwa mwaka 2005,Lakini dr salim aliyeathirika kutokana na kampeni hizo..YUPO SALAMA.
Wanamtandao walishindwa kuelewa na kuchambua hotuba ya mwalimu nyerere ya 1995 kilimanjo hotel/
Kama vikao hivyo vitakapokuwa vimeshindwa kusimamia hili,MAKUNDI NDANI YA CCM HAYATAISHA KABISA,BADALA YAKE CCM ITAKUFA KIFO CHA KUJITAKIA.
Baadhi ya majjina ya wanamtandao waliotia nia ni: Lowassa, Membe, Sitta, Nyalandu, Wasira, Migiro, Mwigulu, January, Ngeleja, Kamani, Kitine, Mbega, Mahiga, Bilal, Kingwangala, Muhongo, Amina Salum, Ally Karume na kadhalika.

No comments: