Translate

Thursday, April 30, 2015

Rais KIKWETE afanya mazungumzo na BILL CLINTON


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kisha kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe Bill Clinton Ikulu jijini Dar es salaam
Rais JAKAYA KIKWETE amekutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa 42 wa MAREKANI - BILL CLINTON ambaye anaendelea na ziara yake nchini. 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais IKULU Jijini DSM imesema kuwa wakati wa mazungumzo yao viongozi hao wamezungumzia baadhi ya miradi inayodhaminiwa na kugharimiwa na Taasisi ya CLINTON. 

Miradi hiyo ni ile iliyopo katika sekta ya afya na hasa katika utoaji wa dawa za kurefusha maisha kwa watu wanaoishi na virusi vinavyosababisha ukimwi, afya za akina mama na jinsi ya kupunguza vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Wasichana 300 waokolewa mikononi mwa BOKO HARAM


Wanajeshi Wa Nigeria
Jeshi la NIGERIA limesema kuwa idadi ya wasichana na wanawake waliookolewa kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam wa BOKO HARAM cha nchini humo imefikia zaidi ya Mia Tatu.

Kwa mujibu wa jeshi hilo, Wasichana na wanawake hao wameokolewa baada ya vikosi vya jeshi hilo kushambulia na kuteketeza ngome iliyokuwa imesalia ya Wanamgambo hao katika msitu wa SAMBISA.

Hata hivyo wasichana na wanawake waliookolewa sio wale waliootekwa nyara mara baada ya Wanamgambo wa Kiislam wa BOKO HARAM kuvamia shule moja ya wasichana iliyoko katika jimbo la CHIBOK.

Saturday, April 18, 2015

Faida za tikikiti maji kiafya


Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi.

  • Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika.
    Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.

Saturday, April 4, 2015

Tarehe ya upigaji kura ya maoni yasogezwa mbele


Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC imetangaza kusogeza mbele upigaji kura ya maoni iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 30 April mwaka huu mpaka hapo zoezi la kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura litakapokamilika. 

Tanzania kuwa kituo cha usuluhishi

Map of tanzaniaImage result for Tanzania
Kwa ufupi
Ni wa migogoro ya kibiashara katika sekta ya uwekezaji wa mafuta na gesi.
Dar es Salaam. Tanzania inatarajia kuzindua kituo cha kimataifa cha usuluhishi wa migogoro ya kibiashara kutokana na kukua kwa sekta ya uwekezaji ikiwamo mafuta na gesi nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisema kituo hicho kitazinduliwa Juni mwaka huu na kitasimamia na kutatua migogoro yote ya kibiashara itakayojitokeza katika kipindi hiki cha ugunduzi wa gesi na mafuta.