Translate

Saturday, April 4, 2015

Tarehe ya upigaji kura ya maoni yasogezwa mbele


Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC imetangaza kusogeza mbele upigaji kura ya maoni iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 30 April mwaka huu mpaka hapo zoezi la kuandikisha wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura litakapokamilika. 

Akitangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari jijini DSM Mwenyekiti wa NEC Jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA amesema upigaji kura ya maoni kunategemea kukamilika kwa uandikishaji wa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajiwa kukamilika Mwezi JULAI mwaka huu. 
Jaji Mstaafu LUBUVA amesema kwa mujibu wa sheria tarehe ya upigaji kura itatangazwa baada ya kushauriana na tume ya uchaguzi ya ZANZIBAR -ZEC. 
Kuhusu mashine za kuandikishia wananchi Jaji LUBUVA amesema mashine zote zimekwishalipiwa na zinatarajiwa kuingia nchini wiki ijayo. 
Jaji LUBUVA pia amezungumzia katiba itakayotumika katika uchaguzi mkuu ujao hapa nchini kuwa ni katiba ya sasa kwakuwa Katiba mpya hata ikipitishwa itatakiwa kupitia kipindi cha mpito kabla ya kuanza kutumika.

No comments: