Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye alisema kituo hicho kitazinduliwa Juni mwaka huu na kitasimamia na kutatua migogoro yote ya kibiashara itakayojitokeza katika kipindi hiki cha ugunduzi wa gesi na mafuta.
Saturday, April 4, 2015
Tuesday, March 31, 2015
Wasambaza picha za ngono kufungwa miaka saba jela
Dodoma. Leo, Serikali itawasilisha bungeni muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao wa mwaka 2015 kwa hati ya dharura unaoorodhesha adhabu mbalimbali, ikiwamo ya faini ya Sh50 milioni au kifungo kisichopungua miaka saba kwa mtu atakayebainika kusambaza picha za ngono mtandaoni.
Baadhi ya makosa yaliyoanishwa katika sheria hiyo ni kutuma taarifa bila ridhaa ya mtu, kusambaza picha za ngono na za utupu, udanganyifu unaohusiana na kompyuta, makosa yanayohusiana na utambuzi, kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta na kusambaza picha za utupu za watoto.
Tuesday, March 24, 2015
JK awaambia polisi wakae mguu sawa

Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride maalumu wakati wa hafla ya kuwatunukia vyeo maofisa 289 wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory
- Awataka kujiandaa na vurugu zitakazotokea katika uandikishaji wa wapigakura, Kura ya Maoni ya Katiba na Uchaguzi Mkuu
- Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amelikata Jeshi la Polisi nchini kujiandaa kikamilifu ili kukabiliana na vurugu zozote zitakazojitokeza wakati wa uandikishaji wapigakura, upigaji Kura ya Maoni ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu.Akifunga mafunzo ya maofisa warakibu wasaidizi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema dalili zinaonyesha kwamba kuna watu wenye nia ya kuhatarisha amani katika matukio hayo.“Tunayoyasikia na tunayoyaona yanaashiria kuwapo kwa dalili za wenzetu kukwamisha shughuli hizi za kitaifa kwa kufanya vurugu, Jeshi la Polisi jiandaeni na vitendo vyote vitakavyofanywa kwa lengo la kuhatarisha amani,” alisema akijibu maombi ya kupatiwa vifaa yaliyowasilishwa kwake na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu.Alisema Serikali itahakikisha kazi ya uandikishaji katika daftari la wapigakura, upigaji wa kura ya maoni na uchaguzi mkuu vinafanyika kwa amani na utulivu kwa gharama zozote.
Saturday, March 21, 2015
Mariana: Nilikeketa mabinti 20 wakazimia, sasa naelimisha jamii

KWA UFUPI
Zaidi ya wasichana na wanawake milioni 130 katika nchi 29 barani Afrika na Mashariki ya Kati wameshafanyiwa ukeketaji
“Sitaisahau hii siku maishani mwangu, kutokana na mawazo, hofu na kero niliyoipata kutoka kwa mume wangu, watoto na hata majirani zangu ambao baadhi walikuwa wakisema eti nimeua wasichana 20 baada ya kuwakeketa.
Ilikuwa alfajiri nilipoamka na kuanza kazi ya kuwakeketa wasichana hao 20 nilioletewa na wazazi wao. Nilipoanza kuifanya hiyo kazi huku nikiwa tayari nimeshawakeketa wasichana 12, walianza kuishiwa nguvu na baadhi yao walikuwa wakitokwa na damu nyingi tofauti na wasichana wengine ambao nilikuwa nikiwakeketa kabla yao.
Cha kusikitisha zaidi, nilipomaliza kuwakeketa wote 20, hali zao zilikuwa mbaya na baadhi walizimia, huku damu nyingi zikiendelea kuwatoka.
Niliogopa sana…sikujua la kufanya lakini namshukuru Mungu alinihurumia, mabinti wale baadaye walizinduka na kupata fahamu. Tangu siku hiyo, niliapa kuwa sitafanya tena kazi hiyo ya ukeketaji maana niliona sasa kuna hatari ya kuja kuua.”
Hiyo ni kauli ya ngariba mstaafu Mariana Ndama (66), mkazi wa Kijiji cha Ikungi mkoani Dodoma.
Kwa Mariana, tukio hilo alilichukulia kuwa si la kawaida na hata aliwaza kuwa huenda wenzake wamemchezea mchezo mchafu wa kuroga kwa nia ya kutomtakia heri katika kazi yake hiyo.
Anasema ajali hiyo ya ukeketaji ilikuwa ya kwanza kwake tangu alipoanza kazi hiyo mwaka 1965, katika Kijiji cha Puma mkoani Dodoma.
Hakumbuki idadi halisi ya wasichana aliowakeketa kwa sababu hakuwa anatunza kumbukumbu, bali anakadiria kuwa ni zaidi ya 1,000.
Friday, March 20, 2015
Chama cha ACT chamwandalia Zitto makazi
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
KWA UFUPI
- Mbunge huyo alipanga kuliaga bunge na alisema amekwishapata ruksa ya Spika kuwa angesimama bungeni kuwaaga wabunge na wanachama wa Chadema baada ya chama hicho kumtimua uanachama wake hivi karibuni, lakini ghafla mpango huo uliyeyuka kwa kile kilichoelezwa kuwa Spika amemkatalia.
- Dar es Salaam. Pamoja na mpango wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuliaga Bunge kukwama jana, Chama cha ACT- Tanzania kimetangaza kukamilisha maandalizi ya kumpokea mwanasiasa huyo kuanzia leo.
Subscribe to:
Posts (Atom)

