Translate

Tuesday, August 4, 2015

Faida ya Tunda la parachichi mwilini (AVOCADO)



FAIDA YA TUNDA LA PARACHICHI - PEA (AVOCADO)
Ndani ya tunda hili kuna maji kiasi kidogo sana ukilinganisha na matunda mengine lakini kuna mafuta mengi na unaweza kuchanganya kula na tunda lingine kama vile apple, ndizi, chungwa au hata maziwa kwa kutengeneza juisi.

TINDIKALI
Licha ya kuwa na mafuta parachichi lina tindikali (acid) mbalimbali ikiwemo inayojulikana kama amino ambayo husaidia sana kukinga na kutibu maradhi katika mwili wa binadamu. Tunda hili pia lina protini ya kiwango cha juu.
Pia kuna tindikali inayoitwa oleic acid kwenye parachichi ambayo husaidia kukinga magonjwa ya moyo, kiharusi na kansa.

VITAMINI “E” NA B6
Imeelezwa na wataalamu kuwa tunda hili lina kiwango kikubwa cha vitamini E kuliko ile inayopatikana kutoka kwenye mazao ya wanyama.Parachichi lina vitamini hiyo nyingi kuliko inayopatikana katika mayai ambayo yanasifika kwa kuwa na vitamini e, hivyo hii inathibitisha kuwa lina faida kubwa mwilini.

Yemen yakabiliana na waasi wa Houthi



Wanajeshi wa serikali wameanzisha mashambulio makali yenye lengo la kuwafurusha waasi wa Kihouthi kutoka eneo moja lililokuwa kituo cha wanajeshi wa anga huko mjini Aden.
Kuna ripoti kuwa waasi kadhaa waliuawa .
Kituo hicho muhimu kiitwacho Al Anad kilikuwa pia kikitumiwa na majeshi ya Marekani waliokuwa wakitumia ndege zisizo na rubani kuwalenga wanachama wa kundi la Al Qaeda walioko Yemen.

Mawaziri watano waanguka kura za maoni


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu

Kwa ufupi

  • Ni Chikawe, Makalla, Silima, Ole Telele na Mahadhi
  • Pia yumo Katibu wa NEC CCM Muhamed Seif Khatib
  • Profesa Muhongo, Muradi, Mwakalebela, Nape wapita
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kiislamu Kondoa Dodoma, Hamisi Salum akikabidhi kadi ya CCM kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zake kabla ya kupiga kura kumchagua mgombea udiwani na ubunge wa jimbo hilo katika Kituo cha Maji ya Shamba. Awali, kura za kituo hicho zilichomwa baada ya kubainika kuwa na udanganyifu. Picha na Shakila Nyerere .