Liberia kutumia 'Zmapp' kutibu Ebola

WHO imeruhusu dawa ya Zmapp kutumika kuzuia kuenea kwa Ebola nchini Liberia
Jopo la wataalam wa shirika la afya duniani WHO limeamua kwamba watu wanaweza kutumia dawa ambazo hazijajaribiwa katika mwili wa binaadamu kutibu ugonjwa wa ebola,iwapo maagizo fulani yataheshimiwa ikiwemo ruhusa ya mgonjwa.
Tangazo hilo linajiri huku shirika hilo likitangaza kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo imepita watu 1000 na kwamba kasisi wa uhispania aliyeondolewa nyumbani mwake baada ya kuambukizwa ugonjwa huo amefariki.